Orodha mpya ya mabilionea Afrika yamshirikisha Dangote , Mo Dewji na Isabel dos Santos

Aliko Dangote Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtu tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote

Mfanyabiashara Mohammed Dewji kutoka Tanzania ametajwa kuwa miongoni mwa mabilioni 20 wa Afrika katika ripoti ya jarida la Forbes la mwaka 2020.

92彩票网平台Hatahivyo utajiri wa bilionea wa Tanzania Mo umedaiwa kupungua hadi dola bilioni 1.6.

92彩票网平台Katika ripoti hiyo mfanyabiashara tajiri nchini Nigeria Aliko Dangote ameorodheshwa kwa mara ya tisa mfululizo, kuwa mtu tajiri zaidi barani Afrika .

92彩票网平台Dangote mwenye umri wa miaka 62 ambaye anafanya biashara ya Simiti, Sukari na unga wa ngano ana utajiri wa dola Bilioni 10.1.

Pia unaweza kusoma:

92彩票网平台Dangote anafuatiwa na mfanyabiashara wa Misri Nassef Sawaris ambaye aliongeza utajiri wake kutoka dola bilioni 6.3 hadi dola bilioni nane.

Mfanyabiashara huyo anamiliki asilimia 5.7 ya hisa za kamapuni ya viatu ya Adidas . Ongezeko la hisa za Adidas liliomuongezea dola bilioni moja nukta tano katika akaunti yake.

Haki miliki ya picha HAKI MILIKI YA PICHAAFP/GETTY IMAGES
Image caption Bilionea kutoka Tanzania Mo Dewji

Bilionea aliyeorodheshwa katika nafasi ya tatu ni raia wa Nigeria Mike Adenuga ambaye utajiri wake unatokana na sekta ya mawasiliano na mafuta. Kampuni yake ya mawasiliano ya simu Globacom ndio ya tatu kwa ukubwa nchini Nigeria ikiwa na wateja milioni 43.

92彩票网平台Alijipatia utajiri wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 26 akiuza kanda za viatu na vinywaji.

92彩票网平台Bilionea aliyeorodheshwa wa nne barani Afrika ni mfanyabiashara wa almasi na raia wa Afrika Kusini Nicky Oppenheimer.

Nicky ambaye ni mrithi wa mali ya familia yake ya Oppenheimer ana utajiri wa dola bilioni 7.7.

92彩票网平台Familia yake imekuwa ikihusika na uuzaji wa almasi.

92彩票网平台Isabel dos Santos mwenye utajiri wa dola bilioni 2.2 amedaiwa kujipatia utajiri wake wakati babake alipokuwa rais ambapo alijipatia hisa katika makampuni mengi ya Angola pamoja na benki.

Mwanamke huyo ambaye ametajwa kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika amesema kwamba anamiliki hisa kutoka kampuni zilizopo Ureno, ikiwemo Telecom na runinga ya nyaya.

Msemaji wa Isabel aliambia jarida la Forbes kwamba ni mfanyabiashara huru .

Image caption Mwana wa aliyekuwa rais wa Angola Isabel dos Santos ni miongoni mwa watu matajiri zaidi barani Afrika

Watu matajiri zaidi duniani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bwana Arnault anamiliki hisa katika kampuni ya LVMH, Christian Dior na mpinzani wake Hermes

Katika orodha ya watu wanne matajiri zaidi duniani, Bernard Arnault amempiku Jeff Bezos na kuwa mtu tajiri zaidi duniani akiwa na mali yenye thamani ya dola billioni 116.5.

Bernard ndiye mmiliki wa kmapuni ya mitindo ya Louis Vuitton na Sephora akiwa na idadi ya mitindo chapa.

Jeff Bezos anayemiliki mali yenye thamani ya dola bilioni 115.6 alitangazwa kuwa mtu wa pili kwa utajiri zaidi duniani. Bezoz ambaye anatalakiana na mkewe baada ya kuishi pamoja kwa miaka 25 katika ndoa ametangaza kwamba atahamisha asilimia 4 ya hisa zake za Amazon kwa mtalaka wake.

Watatu katika usanjari huo ni Bill Gates mwenye mali yenye thamani dola bilioni 110.6. Yeye na mkewe Melinda wanasimamia wakfu wa Bill na Melinda Gates , ukiwa ndio wakfu mkubwa wa kibinafsi duniani.

92彩票网平台Wakfu huo hufanya kazi kuimarisha hali ya afya duniani mbali na kutoa fursa sawa kwa walimwengu.

92彩票网平台Tajiri wa nne ni Warren Buffett mwenye mali yenye thamani ya dola bilioni 90.6b. Akijulikana kwa jina maarufu kama Oracle Omaha , Buffet ni mmojwapo wa wawekezaji waliopata ufanisi mkubwa zaidi duniani.

Akiwa mwana wa mbunge wa zamani wa Marekani alinunua hisa akiwa na umri wa miaka 11 na kulipa kodi akiwa na umri wa miaka 13.

Orodha ya mabilionea 20 na utajiri wao barani Afrika:

 1. Aliko Dangote $10.1 B
 2. Nassef Sawiris $8 B
 3. Mike Adenuga $7.7 B
 4. Nicky Oppenheimer $7.7 B
 5. Johann Rupert $6.5 B
 6. Issad Rebrab $4.4 B
 7. Mohamed Mansour $3.3 B
 8. Abdulsamad Rabiu $3.1 B
 9. Naguib Sawiris $3 B
 10. Patrice Motsepe $2.6 B
 11. Koos Bekker $2.5 B
 12. Yasseen Mansour $2.3 B
 13. Isabel dos Santos $2.2 B
 14. Youssef Mansour $1.9 B
 15. Aziz Akhannouch $1.7 B
 16. Mohammed Dewji $1.6 B
 17. Othman Benjelloun $1.4 B
 18. Michiel Le Roux $1.3 B
 19. Strive Masiyiwa $1.1 B
 20. Folorunsho Alakija $1 B

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii