Shirika la ndege la Hong Kong laomba radhi kwa kumlazimisha abiria kufanyiwa vipimo vya mimba

Hong Kong Express Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shirika la ndege la Hong Kong laomba radhi kwa abiria

Shirika la ndege la Hong Kong limemuomba msamaha abiria wake baada ya kumlazimisha kufanya majaribio ya ujauzito ili aweze kusafiri kutoka Hong Kong hadi eneo la Marekani.

92彩票网平台Midori Nishida, 25, alikuwa akisafiri kwa ndege ya Shirika la Hong Kong Novemba hadi visiwa vya Kaskazini vya Mariana.

92彩票网平台Pia vimekuwa jambo la kawaida kwa wanawake raia wa kigeni kuzaa kwasababu ya uhakika wa kupata uraia wa Marekani.

Ndege hiyo ilikuwa inataka kuhakikisha sheria za uhamiaji za Marekani zinafuatwa.

Awali, shirika hilo lilisema kwamba ilikuwa ni sehemu ya kuhakikisha kuwa yuko katika hali nzuri kusafiri. Hata hivyo, limeomba msamaha kwa tukio hilo.

92彩票网平台2018, idadi kubwa ya watalii ikilinganishwa na raia walipata watoto katika kisiwa cha Kaskazini vya Mariana kulingana na data za eneo.

92彩票网平台Hii inasemekana ni kwasababu wanawake wengi raia wa kigeni wengi wa kutoka China - ambao wanasafiri hadi eneo hilo kujifungua.

Nini kilichotokea Novemba?

Bi. Nishida, ambaye kwa sasa anaishi Tokyo lakini alikulia Saipan, alikuwa amejaza fomu kabla ya kusafiri na kuonesha kwamba yeye si mjamzito.

92彩票网平台Licha ya hili, wafanyakazi wa ndege hiyo walitaka afanyiwe vipimo kabla ya kusafiri vilivyojumuisha vipimo vya mimba. Kisha akasindikizwa hadi chooni na kupewa kichupa maalum cha kupima mkojo kuangalia kama ni mjamzito.

Vipimo vilipodhihirisha kwamba yuko sawa, aliruhusiwa kuingia ndani ya ndege na kwenda kuona familia yake ambayo imekuwa ikiishi kwenye kisiwa hicho kwa miaka 20.

Bi. Nishida alitaja mchakato alioupitia kama wenye kumfedhehesha na kuvunja moyo na kusema kuwa shirika hilo halikujibu malalamiko yake ya awali.

Shirika hilo linasema nini sasa?

"Tungependa kuomba msamaha kwa yeyote ambaye ameathirika na hili,''Shirika la ndege la Hong Kong limesema katika taarifa ya NBC News.

"Tulianza kuwa makini na ndege zinazo kwenda Saipan tangu Februray 2019, kusaidia kuhakikisha sheria za uhamiaji za Marekani zinafuatwa,'' Shirika hilo limesema, lilifanya hivyo kufuatia wasiwasi ulioibuliwa na maafisa wa visiwa vya Kaskazini vya Mariana.

"Pia baada ya kupitia tena sheria hii tumeamua kuitupilia mbali."


Mada zinazohusiana