Kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Khamenei ametetea majeshi kwa kudungua ndege ya Ukraine

Picha ya Ayatollah Ali Khamenei siku ya Ijumaa Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ayatollah Ali Khamenei ambaye ni kiongozi mkuu wa kidini wa Iran ndiye mwenye usemi wa mwisho kuhusiana na masuala yote ya kisiasa nchini humo

Kiongozi mkuu dini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ametetea majeshi ya nchi yake baada ya kukiri kuwa ilidungua ndege ya abiria ya Ukraine kimakosa.

92彩票网平台Amesema kikosi maalum cha majeshi ya ulinzi ya Iran Revolutionary Guard - kilichohusika na mkasa huo kilikuwa - "kinalinda usalama" wa Iran.

92彩票网平台Maandamano ya ndani ya nchi na ukosoaji kutoka mataifa ya kigeni yameiweka Iran mashakani kuhusisna na jinsi inavyoshughulikia tukio hilo.

Lakini Ayatollah alitoa tamko hilo wakati wa alipoongoza sala ya Ijumaa mjini Tehran kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012.

92彩票网平台Ametoa wito wa "umoja wa kitaifa" na kusema kuwa "maadui" wa Iran - akiashiria Washington na washirika wake - wanatumia ajali hiyo ya ndege kuzima mauaji ya jenerali Qasem Soleimani.

"Mamilioni ya raia wa Iran na maelfu ya raia wa Iraq walimuomboleza [Soleimani]," alisema.

Pia unaweza kusoma zaidi:

Ndege aina ya Boeing 737-800 ya shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilikuwa inasafiri kuelekea Kyiv kutoka Tehran Januari 8, ilipoanguka muda mfupi baada ya kuanza safari.

92彩票网平台Abiria wote 176 waliokua ndani ya ndege hiyo wengi wao raia wa Iranian na Canada, walifariki.

Utawala wa pia uko kwenye shinikizo kutokana na kuporomoka kwa uchumi hali iliyosababishwa na vikwazo vya Marekani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu ya Wairan wakishagilia chini ya bango lenye picha ya jenerali Qasem Soleiman aliyeuawa na Marekani

Ayatollah alisema nini kingine?

Ayatollah Khamenei, 80, alihutubia taifa kutoka msikiti wa Mosalla uliopo mji mkuu wa Tehran.

Mara ya mwisho alifanya hivyo ilikuwa mwaka 2012 wakati wa kumbukizi ya miaka 33 ya mapinduzi ya kiislam katika nchi hiyo.

92彩票网平台Akiwatetea wanajeshi , Ayatollah pia:

  • Alikosoa na kuutaja kuwa wenye "chuki" utawala wa rais wa Marekani Donald Trump
  • Alisema hatua ya Iran kushambulia kwa makombora vituo vya wanajeshi wa Marekani nchini Iraq ilikuwa"kofi la usoni" kuonesha Marekani kuwa"Mungu anaunga mkono" Iran
  • Alielezea kikosi maalum cha Quds - ambacho Marekani imetambua kama shirika la kigaidi - kuwa "shirika la kibinadamu linalothamini utu"
  • Alitaja mazishi ya Soleimani na hatua ya majeshi ya the Iran kama "mwanzo mpya wa kihistoria"

92彩票网平台Siku ya Jumatano, Rais Hassan Rouhani aliomba kuwepo kwa mshikamano wa kitaifa.

92彩票网平台Lakini katika ishara ambazo hujitokeza kwa nadra ndani ya utawala wa Iran, rais Rouhani amelitaka jeshi kuwajibika kwa kutoa maelezo ni kwa vipi waliidungua ndege ya Ukraine.

92彩票网平台Ndege aina ya Boeing 737-800, iliyokuwa ikisafiri kwenda Kyiv ikiwa na abiria wengi waliokuwa wakielekea Canada, iliangukamuda mfupi baada ya kupaa kutoka Tehran, tukio lililogharimu maisha ya watu 176 waliokuwa kwenye ndege.

Kwa siku tatu mamlaka za Iran zilikana kuhusika na tukio hilo lakini baada ya shinikizo kutoka kwa jumuia ya kimataifa, jeshi lilikiri kuwa ndege hiyo ilishambuliwa kimakosa wakati wa msuguano kati ya Iran na Marekani.

Saa chache kabla, makombora ya Iran yalilenga kambi mbili za jeshi la anga nchini Iraq zilizokuwa na wanajeshi wa Marekani.

92彩票网平台Shambulio la roketi lilikuwa kisasi baada ya ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani kufanya shambulizi Baghdad na kusababisha kifo cha jenerali Qasem Soleimani.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii