Kesi ya kumuondoa Trump: Maseneta waapishwa kwa kesi ya kihistoria

Maseneta wa Republican na Jaji mkuu wakiingia kwenye jengo la bunge la Seneti Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maseneta wa Republican na Jaji mkuu wakiingia kwenye jengo la bunge la Seneti

Maseneta 100 wa Marekani wameapishwa Alhamisi kama baraza la mahakama litakaloshughulikia kesi inayomkabili rais Donald Trump.

92彩票网平台Hakimu mkuu wa mahakama ya juu zaidi John Roberts aliapisha maseneta kuhakikisha wanatenda haki bila upendeleo.

92彩票网平台Wiki zijazo, maseneta wataamua iwapo Trump anastahili kuondolewa madarakani kwa makosa yaliyowasilishwa na Bunge la Wawakilishi.

92彩票网平台Kesi hiyo imepangiwa kuanza kusikilizwa Januari 21.

Hakimu Roberts aliwauliza maseneta, " Je munaapa ya kwamba katika kesi inayomkabili Donald Trump, Rais wa Marekani, ambayo inayongoja kusikilizwa, mutatenda haki bila upendeleo kulingana na katiba, Mungu awasaidie?"

Wabunge wakajibu "Ndio" kabla ya kila mmoja wao kusaini kitabu walichochukua nacho kiapo. Kiongozi wa waliowengi wa Republican Mitch McConnell, kisha akaahirisha kikao cha kutathmini iwapo Donald Trump ana kesi ya kujibu na kutangaza kwanza kesi hiyo itaanza kusikilizwa Jumanne, 13:00 EST (18:00 GMT).

Bwana Trump anashtumiwa kwa kutumia vibaya madaraka na kuingilia bunge. Hata hivyo amekanusha kutekeleza makosa hayo na kusema kwamba kesi dhidi yake ni madai ya udanganyifu.

Kilichotokea Alhamisi?

Vikao vya bunge la Seneti vilianza huku msimamizi wa bunge akihakikisha shughuli za bunge ziko sawa (sergeant at arms). Vifungu vya kumuondoa Trump madarakani vilisomwa na mbunge wa Congress na mwendesha mashtaka mkuu Adam Schiff.

92彩票网平台Bwana Schiff ni mmoja kati ya saba ambao watakuwa wanafanya maamuzi ya kesi dhidi ya rais. Alisema hakuna rais ambaye amewahi kuzuia mchakato wa kura ya kutokuwa na imani naye.

92彩票网平台Chuck Schumer, Kiongozi wa Democratic katika bunge la Seneti, alitoa tena wito kwa mashahidi wapya kujitokeza na vilevile ushahidi wa nyaraka uruhusiwe bungeni. ''Kesi hii inahitaji uthibitisho wa wazi.''

Bunge la Wawakilishi limemshtumu rais kwa kujaribu kumkandamaiza kiongozi wa nje kwa manufaa ya kibinafsi," Schumer amesema.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Spika wa Bunge Nancy Pelosi ametaka mchakato wa kesi kufanyika kwa haki

Seneta Susan Collins wa Republican ambaye atakuwa na kibarua kigumu cha kuchaguliwa tena mwaka huu, alionekana akibubujikwa na machozi wakati mashtaka yanasomwa.

Wabunge waandamizi wa Democrats walimkosoa pakubwa McConnell baada ya kuahidi kushirikiana na rais Trump na kuonekana kama anayetangua kiapo walichoapishwa maseneta wa Republican cha kuendeleza kesi hiyo kwa haki na bila upendeleo.

Akizungumza baada ya vikao vya Alhamisi, Bwana Schumer aliwaambia wanahabari: "McConnell amesema kwamba yeye atashirikiana na rais, sisi hatutashirikiana na yeyote."

Schumer amesema anatarajia kwamba wiki ijayo kutapigwa kura ya iwapo mashahidi wataitwa na kuongeza kuwa hajaona azimio la kiongozi wa wabunge wa Republican kuhusu sheria za kufuatwa wakati wa kesi hiyo.

Bwana McConnell hajaondoa uwezekano wa mashihidi kuitwa. Lakini alipendekeza kwamba hilo litakuwa ni sawa na kuigiza kesi ya kutokuwa na imani ya Rais Bill Clinton 1999, wakati ambapo maseneta walipiga kura ya mashahidi watakaoitwa na kufuatiwa na majadiliano makali na kipindi cha maswali yaliyoandikwa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nancy Pelosi

92彩票网平台Wakati kikao hicho kinaelekea kukamilika katika eneo la Capitol Hill, Alhamisi, Trump aliwaambia wanahabari waliokuwa Ikulu kwamba kesi hiyo inastahili kumalizika haraka iwezekanavyo.

92彩票网平台"Huu ni uwongo mtupu," rais amesema. "Madai ya undanganyifu yaliyotungwa na Democrats ili wapate kushinda katika uchaguzi." Alirejelelea kauli yake kwenye mtandao wa 92彩票网平台 na kusema kwamba amefunguliwa kesi ya kumuondoa madarakani kwa kupiga simu ya nia njema.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiongozi wa bunge la Seneti kwa kutoka Democratic Chuck Schumer

Nini kilichotokea?

Democrats wanadai kwamba Rais alizuia $391m (£299m) msaada wa kijeshi ili kushinikiza Ukraine kumchunguza mpinzani wake wa kisiasa, Joe Biden. Trump ni rais wa tatu kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye. Marasis wawili wa kwanza ni Andrew Johnson na Bill Clinton ambao hawakuondolewa madarakani.

92彩票网平台Thuluthi mbili ya maseneta inahitajika ili rais aweze kuondolewa madarakani.

Wakati ambapo Bunge la Seneta linaongozwa na Republican, anatarajiwa kuondolewa mashtaka hayo.

92彩票网平台Timu yake ya utetezi bado haijatangazwa, lakini mawakili ya Ikulu ya Marekani Pat Cipollone na Jay Sekulow wameombwa kuongoza.

Bunge la Wawakilishi lilipiga kura Jumatano kupeleka madai ya kumuondoa madarakani kwa bunge la Seneti, baada ya kupiga kura ya 228-193.

Mada zinazohusiana