Sherehe za Krismasi duniani kwa picha

Kutoka barani AfrikahadiAustralia, misa na sherehe mbalimbali zimekuwa zikifanyika kuadhimisha moja ya siku takatifu katika kalenda za dini ya kikristo. Hizi ni baadhi ya picha zilizopigwa sehemu mbali mbali duniani.

Kenya

Christmas eve vigil mass in the Fort Jesus area of Nairobi, Kenya, December 25, 2019 Haki miliki ya picha Reuters

Jijini Mombasa misa ilifanyika usiku wa manane katika eneo maarufu la Fort Jesus.

uHURU pARK

92彩票网平台Jijini Nairobi mchana watu wakajitokeza kwenye viwanja vya bustani ya Uhuru kusherehekea na familia zao.

uHURU pARK

92彩票网平台Pia ilikuwa fursa nzuri kwa wafanyabiashara kwenye eneo hilo.

Khartoum, Sudani

Christians attend a Christmas Mass at St. Matthew's Cathedral Church in Khartoum Haki miliki ya picha EPA

92彩票网平台Misa ya krismasi ikisherehekewa katika kanisa kuu la mtakatifu Mathayo ndani ya mji mkuu wa Sudani.

Colombo, Sri Lanka

Sri Lankan Catholic children dressed up as angels Haki miliki ya picha EPA

Watoto wa kikatoliki nchini Sri Lanka wakiwa wamevaa kama malaika katika kanisa la mtakatifu Anthony. Katika Jumapili ya pasaka, kanisa hilo lilikuwa la tatu kulengwa na watu waliovaa mabomu ya kujitoa muhanga, watu 54 walifariki dunia hapa, na zaidi ya watu 300 katika sehemu nyingine za nchi hiyo.

Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu

A worshiper lights a candle at St. Joseph"s Cathedral Catholic Church in Abu Dhabi, United Arab Emirates, 24 December 2019 Haki miliki ya picha EPA

Muumini akiwasha mshumaa katika kanisa kuu la mtakatifu Joseph. Falme za Kiarabu ina jamii imayokua ya kikatoliki, huku Wafilipino wakiwa ni asilimia tano ya idadi ya watu wote.

Hanoi, Vietnam

A woman takes a selfie outside . Joseph"s cathedral in Hanoi on December 24, 2019. Haki miliki ya picha AFP

Mwanamke mmoja akijipiga picha nje ya kanisa kuu la mtakatifu Joseph katika mji mkuu wa Vietnam.

Paris, Ufaransa

midnight mass for Christmas at the Saint Germain l"Auxerrois church in Paris, France, 25 December 2019 Haki miliki ya picha EPA

Askofu Pilippe Marsset akiendesha misa ya usiku katika kanisa la mtakatika Germain l'Auxrrois. Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 200, Misa ya krismasi haikufanyika katika kanisa kuu la Notre-Dame baada ya moto mkali kutokea mwezi Aprili mwaka huu.

Bethlehem, Palestina

Christmas midnight mass in the Church of the Nativity, in Bethlehem in the West Bank, 25 December 2019 Haki miliki ya picha EPA

Misa ya usiku ikiendelea katika mji wa Magharibi wa Bank ambako Biblia inasema ndipo Yesu alipozaliwa.

Mji wa Vatican

Pope Francis leads a Christmas Eve mass in St Peter's Basilica Haki miliki ya picha AFP

92彩票网平台 Katika misa yake ya saba ya krismasi, Papa Francis amesema Mungu aliwapenda hata wale walio wabaya kati yetu, ujumbe unaoweza kutafsiriwa kuwa unahusu matatizo ya kanisa.

Aleppo, Syria

Worshippers attend Christmas Morning mass at a Syriac Orthodox Church in Syria"s northern city of Aleppo Haki miliki ya picha AFP

92彩票网平台Misa ya krismasi ya asubuhi ikiendelea katika kanisa la orthodox katika mji wa vita wa Aleppo nchini Syria. Jamii ya kikristo nchini humo ni moja jamii za zamani duniani, ukiridu nyuma hadi milenia mbili. watu wa wengi jamii hii hutokea katika madhehebu ya mashariki. Kanisa la Orthodox la Kigiriki, Kanisa la kitume la Kiarmenia na kanisa la Orthodox la Syria.

Baghdad, Iraqi

Iraqi Christians attend a Christmas Mass at St. George Anglican church in Baghdad Haki miliki ya picha EPA

Nchini Iraqi, wakristo wamehudhuria misa ya krismasi katika kanisa la kianglikana la mtakatifu George, wakati huo huo maandamano yanayoipinga serikali, yaliyoanza mwezi Oktoba yakiendelea. Baadhi wanakadiria kuwa jamii ya kikristo nchini humo imepungua kutoka milioni 1.5 mwaka 2013, hadi kufikia 250,000.

Sydney, Australia

A mural depicting Scott Morrison wearing an unbuttoned Hawaiian shirt Haki miliki ya picha EPA

Katika siku kuu za krismasi picha hii imeonekana mjini Sydney ikimkashifu waziri mkuu Scott Morrison kwa kuchukua likizo ya kwenda Hawaii wakati nchi hiyo ikipambana na moto wa msituni.

Picha zote zina hatimiliki

Mada zinazohusiana