Kesi dhidi ya Trump: Mshirika wa wakili wa Trump adai rais wa Marekani alifahamu njama za kumchafua mpinzani wake

Picha kushoto ni Spika Nancy Pelosi na Kulia ni Rais Donald Trump Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Picha kushoto ni Spika Nancy Pelosi na Kulia ni Rais Donald Trump

Mshirika wa karibu wa wakili wa Rais wa Marekani Rudy Giuliani anadai kuwa Donald Trump "alijua kila kitu kinachoendelea" kuhusu kushinikizwa kwa nchi ya Ukraine kuwachunguza Makamu wa Rais mstaafu Joe Biden pamoja na mtoto wake.

Lev Parnas amekiambia kituo cha runinga cha MSNBC kuwa Guilani alikuwa hachunguzi tuhuma za rushwa bali namna ya kumchafua Biden ambaye anaonekana kuwa kinara wa tiketi ya kiti cha Urais kupitia chama cha Democrats.

Rais Trump anakanusha vikali madai hayo.

Wakati hayo yakijiri, Baraza la Wawakilishi nchini Marekani limepiga kura kuidhinisha kutumwa kwa mashtaka dhidi ya Rais Donald Trump kwenda katika Baraza la Seneti ikiwa ni hatua ambayo inaashiria kuanza kwa kesi inayoweza kumuondoa madarakani.

92彩票网平台Bw Parnas ambaye anakabiliwa na kesi ya jinai amedai kuwa rais Trump anadanganya na anajua wazi masharti waliyopwapa Ukraine kuwa kama usingefanyika uchunguzi dhidi ya Biden na mwanawe Hunter ambaye alikuwa mkurugenzi wa kampuni ya gesi Ukraine, basi msaada wa kijeshi kwa nchi hiyo kutoka Marekani ungesitishwa.

Kesi hiyo imepelekwa Seneti katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja tangu wabunge wa Baraza la Wawakilishi kumkuta na hatia Rais Trump ya matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia juhudi za Bunge kuchunguza vitendo vyake.

92彩票网平台Wabunge wa Baraza la Wawakilishi wamepitisha azimia hilo kwa kura 228 dhidi ya 193. Huku Spika Nancy Pelosi akisaini uamuzi huo sambamba na timu ya Wabunge wa Democratic ambao wataendesha mashtaka ya kesi hiyo inayomkabili Rais Trump.

92彩票网平台Mameneja wameteuliwa leo na spika kwa ajili ya kuendesha mashtaka kutokana na kupeleka ambacho kimepitishwa. masetena kama wazee wa baraza na baadaye kupiga kura.

Baraza hilo la Wawakilishi ambalo linadhibitiwa na chama cha upinzani cha Democrats, kutaka Rais Trump kuondolewa madarakani.

Hata hivyo Baraza la Seneti ambalo linadhibitiwa na chama tawala kinachoongozwa na Rais Trump, kitaamua aidha kumtia hatiani na kumuondoa madarakani. Jambo ambalo halitarajiwi.

92彩票网平台Katika mkutano na wanahabari kabla ya kutia saini hati, Bibi Pelosi alisema: ''Leo tutaweka historia tutakapo peleka hati za mashtaka dhidi ya rais wa Marekani kwa vitendo vyake vya matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia majukumu ya bunge kushughulikia suala hilo''.

92彩票网平台Hati hizo kisha zikapelekwa kwenye baraza la seneti, ambapo kiongozi wake ni Mitch McConnell kutoka chama cha Republican amesema zitawasilishwa siku ya Alhamisi mchana, zoezi litakalofuatiwa na kusikilizwa kesi siku ya Jumanne juma lijalo.

Image caption Donald Trump amekuwa rais wa tatu katika historia ya Marekani kupigiwa kura ya matumizi mabaya ya madaraka

Kama Seneti haitapiga (uwezekano ni mkubwa) kura ya kumvua madarakaTrump, sasa ni nini maana ya mchakato wote huu?

Kama uliwasikiliza Democrats, sababu iliyowafanya wapitie yote haya hata kama mtazamo ni kwamba uwezekano wa Seneti (ambayo inatawaliwa na chama cha Trump, Republican) wa kumpata na hatia ni mdogo sana au haupo ni kwa sababu wanahisi wanawajibu wa kumuwajibisha rais kwa matendo yake.

Wanamtazama rais kama mtu aliyetumia vibaya mamlaka aliyonayo kuishinikiza Ukraine kuanzisha uchungzi dhidi ya hasimu wake wa kisiasa, na kama hawatachukua hatua ,hata kama haitawezesha kuondolewa kwake madarakani , rais atalazimika kuchukua hatua zaidi ambazo zinaweza kuwa na athari kwa Democrat katika uchaguzi wa mwaka huu.

Halafu kuna ukweli halisi wa kisiasa kwamba makao makuu ya Democrat yamekua yakijiandaa kwa uchunguzi huu kwa miezi kadhaa.

Kama maafisa wakuu wa Democrat wasingelichukua hatua, wangekuwa katika hatari ya kuwakosa wafuasi wao au kukabiliwa na changamoto katika uchaguzi wa majimbo au kupoteza ufuasi katika uchaguzi mkuu kwa sababu wafuasi wao wasingehisi kuwa na msukumo wa kutosha wa kurejea katika uchaguzi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii